Na Bukuru Elias Daniel
Mahakama nchini Burundi imeamuru kusalia gerezani kwa waziri mkuu wa zamani wa burundi Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye anashtakiwa kwa shutuma za kuhujumu usalama wa taifa, kumtusi rais.
Bunyoni alikuwa waziri mkuu kuanzia katikati ya mwaka 2020 lakini alifutwa kazi mwaka wa 2022, siku chache baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kuonya kuhusu njama ya mapinduzi” dhidi yake.
Nafasi ya mkuu huyo wa zamani wa polisi na waziri wa usalama wa ndani ilichukuliwa na waziri wa mambo ya ndani jenerali Gervais Ndirakobuca mzaliwa wa Cibitoke magharibi mwa Burundi.