Dereva,Utingo na abiria wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto huku wengine watatu wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha Malori mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la Manzese wilayani Kahama mkoani Shinyanga huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa uzembe na Mwendokasi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha Malori Mawili ya Mizigo Namba T 854 DBY lenye tela namba T 180 DVH likitokea Dar es salam kuelekea Runzewe na Lori namba T 195 EEY Lenye tela namba T 811 DYU.