Wakati baadhi ya Wananchi wakikiri kuwa kuna Watu kadhaa wanahofiwa kufariki kutokana na kupigwa risasi na Polisi wakijaribu kuwatawanya kwenye maandamano yaliyofanywa na Wananchi huko Busega Mkoani Simiyu Agosti 21, 2024, imethibitika kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega Faiza Salim pamoja na Maofisa wengine wamejeruhiwa kwa mawe na Wananchi hao.
Imeelezwa kuwa Wananchi walimrushia Mkuu huyo wa Wilaya mawe wakati akiwasogelea kwa nia ya kuwasikiliza ambapo hawakutaka Kiongozi huyo kufanya chochote na kuanza kumrushia mawe yaliyopelekea kujeruhiwa kwenye ubavu na mgongoni huku Maofisa wengine aliokuwa ameambatana nao ambao ni Kamanda wa Zimamoto Simiyu na Kaimu Afisa wa TAKUKURU Simiyu wakijeruhiwa kichwani na kupelekea kushonwa nyuzi.