Timu ya Coastal Union imeachana na kocha wao David Ouma raia wa Kenya, Ouma na Coastal wamefikia makubaliano ya pande mbili.
Joseph Lazaro na Ngawina Ngawina ndio ambao wamepewa jukumu la kukinoa kikosi cha Coastal Union, wakati wanatafuta kocha mwingine.
Coasta Union hawajacheza mchezo wowote wa ligi kuu Tanzania huku wakitarajia kucheza mchezo wao wa kwanza August 29 vs KMC.
Coastal wanajiandaa na mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika hatua ya awali vs FC Bravos (Angola) unaotarajiwa kufanyika Jumapili ya tar 25 pale Chamazi.