RASMI Simba haitakuwa na nyota wao Michael Fred ambaye alikuwa kwenye kikosi hicho msimu wa 2023/24 kwenye mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.
Ikumbukwe kwamba Michael ambaye alipewa jina la fungafunga anaingia kwenye orodha ya nyota wapya ambao walipata nafasi ya kufunga kwenye Kariakoo Dabi kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya ardhi ya Tanzania.
Ilikuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Simba na bao la Simba lilifungwa na Fred ambaye alianzia benchi kwenye mchezo huo ambao Yanga ilikomba pointi tatu mazima.
Fred kwenye ligialitupia jumla ya mabao sita hakuwa kwenye mechi za kumalizia mzunguko wa pili baada ya kupata maumivu kwenye moja ya mchezo katika mzunguko wa pili.
Amekutana na Thank You rasmi Agosti 22 kwa kuwa alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa na timu kambini nchini Misri kwa maandalizi ya msimu wa 2024/25 ambao tayari umeanza kwa kasi.
Lionel Ateba huyu anatajwa kuwa mrithi wa mikoba ya Fred tayari mambo safi baada ya kukamilisha masuala ya vibali kuitumikia Simba ambayo mchezo wake ujao ni dhidi ya Fountain Gate, Agosti 25 2024 Uwanja wa KMC, Mwenge.
Katika mchezo wa kwanza wa Simba ilikuwa Agosti 18 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 3-0 Tabora United.