Rasmi klabu ya Simba watacheza dhidi ya Al Ahly TRIPOLI ya Libya katika mchezo wa mtoano wa kombe la shirikisho mara baada ya timu hiyo kufanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1 dhidi ya timu ya Uhamiaji kutoka Zanzibar.
Al Ahly TRIPOLI katika historia ya michuano ya kimataifa wamefanikiwa kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika mara 1 mwaka 2017 huku katika kombe la shirikisho wakifanikiwa kutinga nusu fainali mara moja tu mwaka 2022.
Mechi ya kwanza inatarajiwa kufanyika ugenini nchini Libya Septemba 13 ambapo Simba wataanzia ugenini kisha kumalizia nyumbani kwa Mkapa.