Klabu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu ya England ipo tayari kuchukua nafasi kubwa katika kukuza utalii Zanzibar ambapo Mabingwa hao mara mbili wa ligi ya Mabingwa Ulaya wanatarajiwa kuanzisha shule ya kukuza vipaji vya soka visiwani humo.
Hayo yamebainishwa kufuatia kikao kati ya Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Ubia wa Chelsea Barnes Hampel kilichofanyika Ikulu Mjini Zanzibar Alhamisi
Ushirikiano huu kati ya Chelsea na Zanzibar unaashiria ushirikiano wenye matumaini ambao sio tu utaimarisha utalii bali pia utatoa fursa kwa maendeleo ya vijana kupitia vyuo vya soka.