UONGOZI wa Fountain Gate umeweka wazi kuwa una timu bora ambayo italeta ushindani ndani ya ligi licha ya kuanza kwa kupoteza mchezo wao wa kwanza.
Ipo wazi kuwa Agosti 25 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC, Mwenge ulisoma Simba 4-0 Fountain Gate ikiwa ni mchezo wa ligi.
Ofisa Habari wa Fountain Gate, Issa Liponda wengi wanamtambua kwa jina la Mbuzi amebainisha kuwa wanawachezaji wenye uwezo mkubwa kuwapa matokeo kwenye mechi ambazo watacheza.
“Unaona tumepoteza mchezo wetu wa kwanza lakini wachezaji wengi walioanza kikosi cha kwanza wote ni wazawa wapo wengine walikuwa jukwaani kutokana na kukosa vibali mpango ukikamilika tutakuwa imara mashabiki wazidi kuwa nasi.”