UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa mshambuliaji wao Steven Mukwala atafanya kazi kubwa ndani ya uwanja kwa kufunga mabao mengi kwa kuwa anasifa hiyo na uwezo wakutimiza majukumu akishirikiana na wachezaji wenzake.
Ndani ya ligi Mukwala mzee wa Waa alifunga bao moja kwenye mchezo wa pili dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge akitumia pasi ya mzawa Shomari Kapombe.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa kila mchezaji ndani ya uwanja anafanya kazi yake kwa ushirikiano mkubwa jambo linalowapa matokeo hivyo hakuna mashaka juu ya uwezo wa Mukwala.
“Mukwala ni mchezaji mzuri ana uwezo wa kufunga na hilo linaonekana kwenye uwanja.Ikiwa mchezaji ana malengo fulani ya kufunga mabao mengi hakuna matatizo kwani ni muhimu kuwa na malengo na uongozi kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha malengo yake yanatimia.
“Kuna kazi kubwa yakufanya katika eneo la ushambuliaji kwani ili kupata ushindi ni muhimu kufunga.Kwenye mchezo dhidi ya Tabora United ilibidi kutumia nguvu katika kufunga na iliwezekana hivyo bado tuna kazi ya kufanya kwenye mechi zijazo.”
Simba inaongoza ligi baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 imekusanya pointi sita huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 7 na ukuta haujaruhusu kufungwa msimu wa 2024/25.