Umoja wa Mataifa ulisema kuwa Israel imekataa maombi ya kusambaza mafuta katika hospitali zinazohudumu kaskazini mwa Gaza mara tano katika wiki iliyopita.
Hayo yamejiri katika mkutano na waandishi wa habari na msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, ambapo alithibitisha kuwa baadhi ya hospitali kaskazini mwa Gaza zimekuwa hazina mafuta mapya kwa zaidi ya siku 10.
Amedokeza kuwa kuna msongamano mkubwa wa wakimbizi kusini mwa Gaza kutokana na amri zinazoendelea za kuwahamisha Israel.
Katika muktadha mwingine, alieleza kuwa juhudi zinaendelea za kuteua na kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na watu wa kujitolea zaidi ya 1,000 katika vituo 11 vya afya mkoani humo kwa ajili ya chanjo ya polio.
Alisema wanalenga katika duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo kufikia angalau 95% ya zaidi ya watoto 640,000 walio chini ya umri wa miaka 10 huko Gaza.