Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametembelea na kukagua Mradi wa Miji 28 Chato mkoani Geita. Mradi huu una Thamani Bil 38 na unatekelezwa na Mkandarasi Afcon wa India.
Aidha Ziara hii ni matokeo ya Maelekezo ya Maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi aliofanya wilayani Chato tarehe 24/08/2024 na kumpigia simu akimtaka Waziri Aweso kufika na kutembelea Mradi wa Miji28 Chato na kuhakikisha mkandarasi anaongeza kasi ya ufanyaji kazi.
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso ametoa maelekezo mazito kwa mkandarasi na wasimamizi wa Mradi akihimiza kuwa kazi ya utekelezaji wa Mradi huu ifanyike usiku na mchana na kwa kasi kwani ni Mradi tegemeo kwa wananchi wa Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla zaidi akisisitiza usimamizi na ufuatilaji toka kwa watendaji wa Wizara ya Maji waliopewa wajibu huo.
Pia, amemuelekeza mkandarasi kuongeza nguvu kazi katika mradi huo na kutoa nafasi ya ajira kwa vijana wa Chato ili pia nao wanufaike na uwepo wa mradi huu kujipatia kipato na kuongeza kasi ya kazi kama nguvu kazi.