Klabu ya Yanga imewasili nchini Ethiopia kuvaana na CBE mchezo wa raundi ya pili kufuzu hatua za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga wamewasili nchini Ethiopia kwa mchezo huo muhimu utakaopigwa siku ya jumamosi tarehe 14 jijini Addis Ababa na kikosi kimeondoka na baadhi ya wachezaji ambao hawakuchaguliwa timu za Taifa wakati wa michuano ya kufuzu AFCON2025.
Kwa mujibu wa KOCHA Miguel Gamondi amesema wachezaji 14 wamekosekana kwenye kikosi kilichoondoka na wataungana na timu hiyo nchini Ethiopia.Kocha huyo amenukuliwa akisema ratiba hiyo imekuwa ngumu kwake kwani hajapata wasaa mzuri wa kukaa na wachezaji na kujiandaa na mchezo huo muhimu.
Kwa taarifa rasmi kutoka Yanga zinasema Farid Mussa si sehemu ya ikosi hicho kilichoondoka kutokana na majeraha yake ya mguu yatakayomweka nje ya uwanja kwa miezi 2 na wachezaji wengine wote wako safi kwa mchezo huo.Yanga wanatakiwa kushinda mchezo huo muhimu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika