erikali imetoa kiasi cha shilingi Milioni 400 kwenda MSD fedha kutoka Serikali kuu na Mapato ya Ndani Halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara ili kununua vifaa tiba kwa ajili ya zahanati14 kwa lengo la kupunguza changamoto katika zahanati hizo ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma karibu na wananchi.
Akiongea na Wananchi katika Zahanati ya Itandura, Nyabitocho, Matamankwe na Korotambe Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara alisema kuwa tayari vifaa vyenye thamanani ya shilingi Milioni 169.77 vimepelekwa Zahanati 14 na wanasubiri Vifaa bakia vyenye thamani ya Shilingi Milioni 231 ili kufikisha Milioni 400 zilizotengwa.
“Serikalikuu pamoja na Halmashauri ya Tarime vijijini kupitia mapato yake ya ndani tumepeleka fedha kiasi cha shilingi Milioni 400 MSD ili walete vifaa tiba kwa lengo la kupunguzia wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya Afya na wakati mwingine kusababusha vifo vya akina mama wakati wa kijifungua kwa sababu ya kukosa madawa muhimu”, alisema Waitara.
Mbunge anasistiza wananchi sasa kutunza maeneo ili yasiwe na Migogoro kwani baadae Zahanati hizo zitapandishwa hadhi hivyo sasa kuna haja kubwa ya kutunza Maeneo yaliyotengwa na serikali.
Willian Matiko ni diwani kata ya Susuni alisema kuwa Zahatati ya Matamankwe ilifunguliwa rasmi mwaka 2022 baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya kazi lakini baada ya kupaza sauti tayari inatoa huduma kwa wananchi na sasa serikali imepeleka vifaa vya kutosha na dawa zote Muhimu zipo.
“Zahanati hii imepokea fedha na kununua Viti na Meza ambavyo vilikuwa changamoto na tayari tulipokea Milioni 40 kwa ajili ya Ukarabati na sasa kichomeataka ujenzi unaendelea hivyo natumia nafasi hii sasa kushukuru Serikali kwa kuleta karibu huduma za wananchi”, alisema Diwani Matiko.
Vile vile Diwani aliongeza kuwa licha ya kuletwa kwa vifaa tiba bado kuna changamoto ya ukosefu wa Nyumba za Waganga nakuomba sasa serikali kuweka nguvu kubwa ili kutatua chagamoto hizo za ukosefu wa Nyumba za watumishi maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Yusuph Sanga ni Mganga Mfawidhi zahanati ya Matamankwe alisema kuwa wamepokea Vitanda vine vukiwemo Viwili kwa ajili ya akina Mama Kujifungua na viwili kwa ajili ya Uchunguzi,Vifaa kwa ajili ya akina mama kujifungua salama,Mzani wa kupima Uzito watoto Wachanga, pamoja na Magodoro.
Yuuph aliongeza kuwa pia jengo la Zahanati ya Matamankwe ni Chakavu pia Vyoo vya Wagonjwa na Watumishi siyo bora nakuomba sasa kutatua changamoto pamoja na upungufu wa mabenchi kwani kuna siku wagonjwa wanakuwa Wengi nakukosa sehemu ya kukaa wakiwemo wajawazito.
Joyce Nyankaira ni Mkazi wa Kiongera alisema kuwa walikuwa wakitumia gharama kubwa zaidi ya shilingi 20,000 kufuata huduma ya Afya kituo cha Afya Sirari hivyo uwepo wa Zahanati hiyo na serikali kuleta vifaa tiba sasa imekuwa mkombozi kwao.
“Akina mama tulikuwa tunajifungulia njiani wakati tukienda Sirari au Mjini Tarime lakini sasa Zahanati yetu ipo karibu na Waganga wapo japo hawana Nyumbaza kulala wanakaa mbali mfano mgonjwa akiletwa usiku ni chnagamoto kubwa sana lakini tunashukuru” alisema Nyanakaira.
Serikali ya Tanzania kupitia Sera ya Afya 2007 imewekeza sana katika kuboresha uhai wa mtoto kupitia utoaji wa huduma bure za afya kwa kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
Mpango Mkakati wa Taifa wa Kuboresha Afya ya Uzazi, Mzazi, Mtoto, na Vijana nchini Tanzania (2016-2020) umeweka mazingira wezeshi ya kupunguza magonjwa, vifo vya akina mama, watoto wachanga, watoto na vijana kwa kutoa huduma bora, endelevu na jumuishi zinazowafikia watu wote katika ngazi mbali mbali za utoaji huduma katika vituo vya afya na kwenye jamii.
Hivyo basi matokeo ya afya za wanawake na watoto yameendelea kuwa bora hivyo kutolewa sasa kwa vifaa tiba hivyo katika Zahanati 14 Halmashauri ya wilaya ya Tarime ni moja ya utekelezaji wa sera za Taifa zilizowekwa.
.Taarifa za tafiti za TDHS-MIS za 2015-16 zinaonesha mafanikio makubwa ya asilimia 98.9 ya mahudhurio ya mama wajawazito waliohudumiwa na wataalamu mwenye ujuzi kutoka asilimia 96 mnamo mwaka 2010.
Mwelekeo wa chanjo za msingi kwa watoto wenye umri wa miezi 12-23 nao unaonesha ongezeko kutoka asilimia 71 mnamo mwaka 2010 hadi asilimia 75 mnamo mwaka 2015/2016 hivyo sasa serikali haina budi kuendelea kuwekeza katika ununuzi wa vifaa tiba pamoja na madawa muhimu katika zahati zinazojengwa kwa sasa.
.Uwekezaji wa Serikali katika uhai wa mtoto unaonekana dhahiri kwenye kupungua kwa vifo vya watoto kati ya mwaka 2010 na 2015 ambapo kiwango cha vifo vya watoto wachanga (0 28 days) vimepungua kutoka vifo 40 hadi 25 kwa kila vizazi hai 1,000, kiwango cha vifo vya watoto wachanga (28 days – 11 months) kupungua kutoka vifo 99 hadi 43 kwa kila vizazi hai 1,000; na kiwango cha vifo vya watoto chini ya miaka 5 (12-59 months) vimepungua kutoka vifo 147 hadi 67 kwa kila vizazi hai 1,000.
Kinacholeta wasiwasi ni kwamba mafanikio ya awali katika afya ya mama na ustawi yameonekana kuongezeka kwa uwiano wa vifo vya akina mama kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mnamo mwaka 2015/16 ikilinganishwa na vifo 454 kwa kila vizazi hai 100,000.
Aidha, inataarifiwa kuwa karibu asilimia 60 ya vifo vya akina mama na karibu robo tatu (asilimia 75) ya vifo vya watoto wachanga hutokea wakati wa wiki ya kwanza baada ya kujifungua.
Aidha, takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa jumla ya asilimia 66 ya akina mama hawapati huduma inayopendekezwa ndani ya siku 2 baada ya kujifungua29 hivyo sasa serikali iwekeze sana ili kuokoa watoto hao kuanzia miaka 0-8.
Halmashauri ya wilaya ya Tarime ina Hospitali moja Vutuo vya Afya 08 na Zahanati 43