Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe ,Dr Benson Bagoza ameipongeza serikali kwa kuhakikisha inarudisha Kodi za wananchi kwa kutekeleza miradi ya kisasa ya barababara.
Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa barabara iliyotengenezwa kwa kiwango cha lami yenye mita 700 Kishao_ Lukajange ambapo amesema kuwa serikali imeendelea kuwa na uaminifu wa kukusanya fedha za wananchi na kuzirudisha katika jamii kwa kutekeleza miradi imara ikiwemo barabara nzuri.
Amesema barabara hiyo ambayo inaelekea katika makao makuu ya Dayosisi ya Karagwe imekuwa kiunganishi kikubwa kati ya wananchi na waumini na kuondoa vikwazo kwa wanachi ambao zamani walishindwa kuudhuria ibada kwa kisingizio Cha matope , huku akisema kuwa baada ya barababara hiyo kukamilika wananchi wamejitokeza kuboresha huduma za migahawa na maduka ya kisasa na wateja wao wanapata huduma nzuri katika mazingira safi.
“Kazi kubwa ya Mwenge wa Uhuru ni kumulika miradi na kuzindua naungana na Kila mtu kutambua kazi kubwa ya TARURA, wanafanya kazi nzuri ,miradi ya viwango,ombi langu kwa serikali ni kuwa mwenge wa Uhuru kwa sasa umulike maaadui wetu tulionao ndani ya nchi”alisema Bagonza.
Mkimbiza mwenge kitaifa Godfrey Mnzava akipongeza hatua za manunuzi zilizofanywa na TARURA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo huku akisema kuwa ,mfumo wa manunuzi wa Kidigtal ambao umepunguza mianya ya Rushwa na kuweka wazi wadhabuni wenye sifa za kutekeleza miradi ya barabara.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Karagwe Kalimbula Malimi amesema kuwa mradi huo umetekelezwa kwa thamani ya shilingi Milioni 385 kwa lengo la kuboresha huduma za kiuchumi kwa wananchi na kupendezesha eneo la mjini huku chanzo Cha fedha hizo ikiwa ni tozo.