Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Mtyangimbole, Halmashauri ya Madaba, Wilaya ya Songea, baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Maji wa Mtyangimbole, kwa niaba ya miradi mingine ya maji 30 inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wa Ruvuma, leo tarehe 24 Septemba 2024, akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.