Tanzania imekuwa mwanachama wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) kwa takribani miaka 50 sasa na kumekuwa na juhudi za uboreshaji wa Sera ya Taifa ya Usafiri kwa njia ya maji unaoendelea nchini na hii imekuwa ishara tosha ya dhamira ya serikali kuboresha usalama wa usafiri kwa njia ya maji.
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi Bi. Stella Katondo katika maadhimisho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji na miaka 50 ya IMO kwa siku ya pili amesema katika kuona hilo elimu zaidi inapaswa kutolewa kuhusu usalama na kuwa na vifaa okozi wakiwa safarini alipotembelea wavuvi wa mwalo wa Makoko mkoani manispaa ya musoma mkoani Mara.
‘ vyombo vya usafiri majini vinatakiwa kukaguliwa kabla ya kuanza safari iwe ya Uvuvi au kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine hiyo ndio sababu wao kutoa elimu kwa wavuvi katika mwalo huu ndio maana tumewafuata kuwapa elimu kwanini ni muhimu kuwa na vifaa vya kuokoa ”
‘Usafiri wote wa majini katika kuwa salama wanatakiwa kuwa na vifaa kinga pale panapo tokea janga lolote kuweza kusaidia kujiokoa katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wanavyotumia vyombo vya usafiri majini’.
Bw. Augustino Magele Kaimu kamanda zimamoto mkoani amesema kuwa ni muhimu katika wavuvi, manahodha wa vyombo, wamiliki wa vyombo, wafanyabiashara na watumiaji wa vyombo vidogo vya usafiri majini kuipata elimu ya jinsi ya kutumia vifaa vya uokoaji pindi inapotokea dharura au ajali majini; utumiaji vifaa vya uokoaji pamoja umuhimu wa kuwa na vifaa vya uokozi kwenye vyombo vya maji.
‘kuwa vifaa vya uokozi katika safari za majini ya uvuvi na safari za kawaida huvaliwa kabla ya safari kuanza kutokana na vifaa hivyo kuendelea kuwepo bila kuvaliwa wakati janga linapotokea hakuna hata mmoja anaweza kukumbuka uwepo wa vifaa hivyo na kusababisha madhara makubwa ikiwemo na vifo lakini mnaweza kupiga mamba za dharura endapo shida ikitokea’.
Bw Mauna Shabani moja ya wavuvi waliohudhuria kupata elimu hii amepongeza na kushukuru juhudi za utoaji elimu na kuomba Shirika kuendelea kufanya hivyo mara kwa mara ili kuongeza uelewa mpana kwa wananchi juu ya sekta ya usafiri majini.
Kilele kikitarajiwa kuwa tarehe 26 Septemba 2024. Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni “Navigating the future:safety first”