Rais mpya wa nchi anatazamiwa kurithi mikoba ya Yoon Suk Yeol aliyeondolewa kutokana na agizo lake la kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi mwishoni mwa mwaka uliopita.
Mpaka sasa duru zinasema kiongozi wa upinzani wa mrengo wa kushoto Lee Jae-myung ndiye aliyeko katika nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi huo.
Mgombea mkuu wa kihafidhina,Kim Moon Soo, anashikilia nafasi ya pili na mshindi anaweza kutangazwa siku ya Jumatano.
Uchaguzi huu utaamua hatma ya demokrasia ya Korea Kusini ingawa wachambuzi wana wasiwasi kwamba mgawanyiko wa ndani uliosababishwa na rais Yoon Suk Yeol bado haujaisha na unaweza kuendelea kuitibua nchi hiyo hata baada ya kupatikana kwa rais mpya.