
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga raia wa Burkina Fasso, Stephene Aziz Ki anatajwa kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaokuja mkwanja mrefu kutokana na thamani yake kuendelea kupaa juu.
Nyota huyo kwa sasa hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26 baada ya kupata changamoto mpya nchini Morocco ambapo amepata dili jipya.
Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo kwenye upande wa mkwanja atakuwa anakunja Sh 1.2Bil kwa mwaka kama sehemu yake ya mshahara hiyo ni kuweka kando mkwanja wake wa usajili ambao amevuta mezani.
Aziz Ki ni dili la miaka miwili amesaini Wydad Athltic Club huku ikielezwa kuwa atakuwa analipwa mshahara wa zaidi ya milioni 88 kwa mwezi, ambao utamfanya akunje zaidi ya bilioni kwa mwaka.
Ikumbukwe kwamba kutakuwa na bonasi ambazo atakuwa anakuja Aziz jambo litakalomfanya awe anavuta mkwanja mrefu kwa mwaka.
