Mtandao wa kijamii wa Whatsapp umeanza kuyaruhusu mashirika kadhaa kufanya majaribio ya mfumo wake mpya ujulikanao kama ”Channel” ambao unayawezesha mashirika hayo kurusha matangazo kwa wafuasi wao kwenye mtandao huo.
Hilo linafanyika wakati kampuni kadhaa zikionyesha kuchoshwa na changamoto za kiufundi zinazouandama mtandao wa Twitter tangu ulipoanza kumilikiwa na bilionea Elon Musk. Kampuni ya Meta inayomiliki Whatsapp imesema mfumo wa Channel ni rahisi na wa kuaminika, kuweza kutumiwa kwa mawasiliano binafsi kati ya watu na mashirika.
Mfumo wa Channel unaweza kutumiwa kubadilishana habari
Kulingana na vidio iiyosambazwa na kampuni ya Meta, mfumo wa Channel katika mtandao wa Whatsapp unaweza kutumiwa kubadilishana habari juu ya matokeo ya michezo na mashindano, hali ya hewa, na hata mbinu za mapishi na kukarabati vifaa vya nyumbani.