Rais Samia amemteua Frank Kanyusi Frank kuwa Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Kabla ya uteuzi Bw. Frank alikuwa Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na anachukua nafasi ya Angela Kemanzi Anatory ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Juni 11, 2023, ambapo pia amemteua Irene Joseph Lesulie kuwa Naibu Kabidhi Wasii Mkuu, kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mashauri ya Kimataifa, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Bi. Irene anachukua nafasi ya Lina Robert Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.