Bunge limeahirisha kwa muda kikaochake kilichokuwa kinaendelea leo Jumanne Juni 27, 2023 baada ya king’ora kinachoashiria kuna jambo la hatari kupiga kelele ndani ya ukumbi.
Ilikuwa ni saa 3.50 asubuhi wakati wabunge wakiendelea kwenye kipindi cha maswali na majibu ndipo king’ora kikalia na Spika, Dk Tulia Ackson akaahirisha shughuli za Bunge.
“Waheshimiwa wabunge hiyo sauti inaashiria tutoke humu ndani kwa haraka sana, kila mmoja atafute mlango wa kutoka na sote twendeni lile eneo la kukusanyikia, naahirisha shughuli za Bunge hadi hali itakapotulia,” amesema Spika Dk Tulia.
Hata hivyo Bunge larejea