UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa eneo ambalo wanalifanyia kazi kwa sasa ni eneo la ushambuliaji ambapo wapo chimbo kusaka mchezaji atakayeongeza nguvu kwenye eneo hilo.
Ipo wazi kwamba ndani ya 2024/25 Simba kwenye Ngao ya Jamii imegotea nafasi ya tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Katika mechi mbili ambazo ni dakika 180, safu ya ushambuliaji ya Simba inayoongozwa na Joshua Mutale shambuliaji refu kuliko goli ni bao moja ilifunga huku ukuta ukiruhusu bao moja pekee kwenye nusu fainali dhidi ya Yanga.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wanatambua kuna ushindani mkubwa ndani ya ligi na kikosi chao ni bora watafanyia maboresho eneo la ushambuliaji.
“Kuna wachezaji bora na wanaokwenda kuipmbania Simba hilo lipo wazi ila viongozi wanafanyia kazi kwenye eneo la ushambuliaji ambalo hilo linahitaji maboresho kuwa bora zaidi, mashabiki wa Simba tuzidi kuwa pamoja kwani furaha inakuja.”