Rais Samia Suluhu Hassan ameteua Wakuu wa Taasisi mbalimbali kama ifuatavyo; Dkt. Irene Isaka ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Crispin Chalamila ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Kabla ya uteuzi alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu
Vilevile, Moremi Andrea Marwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Awali alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza (SHIMA)