Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kusafiri leo Agosti 15 kuelekea Harare, Zimbabwe ambako atashiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Katika Mkutano huo utakao fanyika Agosti 17, Rais Samia atapokea kiti cha Uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kutoka kwa Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema.