Klabu ya Simba Queens imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya CAF Champions league Women qualifier kanda ya CECAFA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kawempe Muslim Ladies Football Club. Simba ilifunga bao lake la kwanza kupitia kwa Corazone Vivian,Bao la pili likifungwa na Jentrix Shikangwa na bao la tatu likifungwa na Elizabeth Wambui.
Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Juma Mgunda kilianza Caroline Rufa eneo la golini ,mabeki wakiwa ni Fatuma Issa,Wincate Kaari,Ruth Ingosi na Violeth Nicholaus. Eneo la kiungo liliundwa na Vivian Corazone,Elizabeth Wambui ,Precious Christopher na Asha Djafari. Eneo la ushambuliaji liliundwa na Jentrix Shikangwa na Asha Rashid.
Kocha Mgunda alifanya mabadiliko madogo eneo la kiungo kwa kutowaanzisha Ritticia Nabossa pamoja na Amina Bilal walioanza mchezo dhidi ya Fad Djibouti mchezo uliomalizika kwa Simba kushinda mabao 5-0 .