Timu ya waokoaji mjini Gaza imesema mashambulizi mabaya ya Israel katika ukanda huo yamesababisha mauaji ya watu 52, huku 33 wakijeruhiwa.
Msemaji wa taasisi ya ulinzi wa raia Mahmud Bassal amesema shambulizi hilo lilitokea katika shule ya Fahmi Al-Jar-jawi. Ameongeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa ni wanawake na watoto.
Hata hivyo jeshi la Israel limesema eneo hilo lilikuwa linawahifadhi magaidi waliokuwa wakishirikiana na kundi la Hamas.
Wakati Israel ikiimarisha mashambulizi yake ya kulisambaratisha kundi la wanamgambo wa Hamas, viongozi wa dunia wanaokutana uhispania watoa wito wa usitishwaji vita, makundi ya kutoa misaada ya kitu yakisema misaada inayotolewa haitoshi kuwafikia watu wa Gaza wanaokumbwa na njaa na changamoto za kiafya.