Na Bukuru Daniel – Burundi
Idadi ya wakimbzi wanaorejea nchini kutoka uhamishoni imepungua ikilinganisha na siku zilizopita.Baadhi yao wanasema kuwa usalama mdogo unaoripotiwa nchini Burundi ndio unaosababisha wasirejeee nchini.
Hata hivyo naibu waziri wa wizara ya mambo ya ndani Jenerali Bonasinze Celestin amesema kuwa wanaorejea nchini hupokelewa kwa furaha na kuwataka wakimbizi wengine kurejea kwa ajili ya kuijenga nchi.