Klabu ya Singida Fountain Gate imetangaza kuachana na Kocha, Hans Van der Pluijm ambapo nafasi ya Kocha Mkuu imekabidhiwa kwa Msaidizi wake, Mathias Lule hadi hapo Uongozi wa Klabu utakapofanya maamuzi tofauti.
Taarifa ya Singida imeeleza maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya Pluijm kuamua kujiuzulu mwenyewe kutokana na sababu binafsi.
Singida ni moja ya timu iliyotumia kiasi kikubwa cha Fedha kusajili wachezaji wenye uzoefu wa mashindano mbalimbali lakini imekuwa na matokeo ya kusuasua tangu kuelekea na hata baada ya kuanza kwa msimu wa 2023/24