Na Bukuru Elias Daniel
Mamlaka nchini Burundi imetangaza bei mpya ya mafuta ikiwa ni mara ya tatu bei inapanda ndani ya miezi mitano.
Bei ya petroli, mjini imepanda kutoka 4450 hadi 4550 faranga ya Burundi, dizeli kutoka 4135 hadi 4150 na mafuta ya taa ikapanda kutoka 4250 hadi 4395.
Waziri wa biashara amesema kupanda kwa mafuta, kumechangiwa na kuongeza kwa gharama ya uagizaji na usafirishaji wa mafuta kutoka soko la kimataifa.